MHANDISI AWEKWA NDANI KWA KUJENGA JENGO LA CHUO CHA MKWAWA CHINI YA KIWANGO
Mahakama imemsomea mashtaka matatu na kumnyima dhamana Mhandisi, Godwin Mshana aliyekamatwa kwa kudaiwa kujenga ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa(MUCE) chini ya kiwango
-
Arudishwa mahabusu baada ya kunyimwa dhamana
-
Mhandisi huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MNM Engineering Service Ltd, mashitaka aliyosomewa ni pamoja na kugushi nyaraka mbali mbali na uhujumu uchumi
-
Rais Magufuli akiwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi aliviagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi wa thamani ya fedha iliyotumika kujenga ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Mkwawa (Muce)
-
Siku kadhaa baada ya agizo hilo Jeshi la Polisi mkoani humo lilimkamata Mkandarasi wa aliyepewa tenda ya Ujenzi wa jengo hilo kwa tuhuma za kufanya kazi chini ya kiwango
Hakuna maoni