Recent Posts

Breaking News

Mwanamke na Uongozi yahamasisha wasichana wa vyuo vikuu kushiriki na kugombea nafasi za uongozi.


Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mh. Sophia Mjema. Ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Mwanamke na Uongozi lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Tarehe 01. 04. 2017.

Katika Kongamano hilo, lililoandaliwa kwa dhamira ya kuwahamasisha wasichana waliopo vyuoni, kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Mama Sophia Mjema, aliwasihi wanawake kutokuwa nyuma na kutokuogopa kushiriki katika masuala ya uongozi katika nafasi mbalimbali.

Aidha, aliwashawishi wasichana wa Elimu ya Juu kujaribu kufuata nyayo zake katika kugombea na kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi tangu akiwa katika Elimu ya Sekondari.

Mkurugenzi na mwanzilishi wa taasisi ya Mwanamke na Uongozi. Bi. Shamira Mshangama akielezea kwa undani kuhusiana na kongamano la Mwananke na Uongozi.



Dr. Kafanabo Mkurugenzi wa kituo cha jinsia (Gender centre ) Chuo Kikuu cha Dar es salaam . Akizungumzia kwa upana suala la Mwanawake na Uongozi.


Mlezi wa Wanafunzi (Dean of students) Wa chuo kikuu cha Dar es salaam.  Dada Paulina Mabuga naye alikuwa  mmoja wa wahudhuriaji na mzungumzaji katika kongamano la Mwanamke na Uongozi.


Irene Ishengoma ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi chuo Kikuu cha Dar es salaam mwaka 2015-2016, alikuwa mzungumzaji aliyewahusia wanawake kujitokeza kwa wingi kutokuwa na woga wa kugombea nafasi za juu za Uongozi wawapo vyu




 Pichani ni baadhi ya matukio mbalimbali ya kongamano la Mwanamke na Uongozi lililofanyika katika ukumbi wa NKRUMAH Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Hakuna maoni