Recent Posts

Breaking News

WITO KWA VIJANA WA CUF (JUVICUF)



Chama ni taasisi inayokusanya watu wenye mawazo tofauti, vipawa tofauti na uwezo tofauti hata hulka tofauti...sio private entity (mali binafsi) kama alivyo kuwa anafanya na anavyotaka lipumba kukifanya chama hiki (CUF) kuwa hivyo.

Aidha, tulio salama tujitahidi kutojigeuza kuwa na fikra za hovyo hovyo kama hizo...za chama kufuata fikra za mtu mmoja (Lipumba) na kupuuza mawazo na maamuzi ya ki-taasisi.

Chama chetu kinafuata misingi na imani ya kiliberali ambayo inaaamini katika mambo makuu manne, na nayarejea ili kuweka kumbukumbu sawa.

1. Rule of law ( utawala wa sheria) constitutionalism..

2. Respect of human rights ( kuheshimu haki za kibinadamu). Kuheshimu tofauti za mawazo (fikra), itikadi na maono, lakini yasiwe kinyume na utaratibu mliojiwekea kama Taasisi.

3. Free trade economy ( uchumi wa soko huru (huria).

4. Inclusive democracy ( demokrasia shirikishi).

Naomba Leo niwakumbushe haya pekee..tujadili bila kushutumiana tukijua kwamba, sote tuna wazo moja na nia yetu ni moja kukihami na kukilinda chama chetu dhidi ya maccm na kundi la watu ndani ya Chama (lipumba) lililopandikizwa kwa kazi maalumu, ili kudhohofisha mapambano yetu kwa ajili ya Taifa hili, kama ambavyo imani yetu kama liberal party tunavyo amini.

Kutumia nguvu, matusi, utekaji, ilimradi tu, Lipumba awe mwenyekiti! Kinyume na maamuzi ya kidemokrasia ndani ya chama, sawasawa na msingi wa Taasisi yetu, ni kushiriki moja kwa moja kuhujumu malengo yetu kama Taasisi, na kwa vyovyote vile, tunakuwa tunageuka kuwa adui wa wenye Chama na Taifa kwa ujumla.

Pia, ni ubinafsi na ulimbukeni wa kupindukia, kwamba, watu woote waamini katika mtu mmoja, ambaye kwa kipindi cha miaka 20 alipokuwa madarakani, ame-prove failure... Hiki ni Chama, haiwezekani kikaongozwa na fikra za mtu mmoja, tutawezaje kujitofautisha na CCM?

Mimi kama kiongozi na kijana, Natoa rai kwa viongozi wa vijana nchi nzima,  wa chama Changu, CUF, Juvi-Cuf, kujitofautisha na kujipambanua kama viongozi. Vijana woote kwa ujumla ni wakati sasa, wa kujitenga na kundi la watu ambao mpaka leo, hakuna mtanzania asie jua kwamba wanatumika, kudhohofisha Chama chetu (CUF) na kudhohofisha mapambano ya haki na demokrasia nchini.

Tunavyo endelea kushindwa kujitenga na lipumba na genge lake, ni kuonyesha wazi kwamba, hatujui nini maana ya kuwa viongozi au hatujitambui kama vijana na umuimu wetu katika Taifa hili, ni kuendelea kudharau dhamana ya mamilioni ya vijana ambao sisi kama taasisi tuko mbele yao.

 Tujielimishe na kuwaelimisha vijana wetu, kwamba tuna adui ndani yetu, anahujumu malengo makuu ya Taasisi yetu na ni wajibu wetu kama vijana kumkataa na kumpinga hadharani kwa nguvu zote.

Kama sisi kama Vijana, tukishindwa kusimama, nani atasimama? Taifa lenye idadi ya vijana zaidi ya asilimia 60, ni Taifa ambalo kwa vyovyote vile linategemea nguvu ya vijana. Na vijana ndio sisi, ni lazima tujitambue.

Tangu Lipumba kwa msaada wa dola, aendelee kufanya shughuli za Chama, kwa baadhi ya maeneo, ni kipi kama faida kwa Chama, na Taifa kwa ujumla, tumeipata? Zaidi ya kuuthibitishia umma namna ambavyo anafanya kazi za ccm dhidi yetu!!

Kuna faida gani so far, tumeipata kama Taifa, Kama Chama, tumeipata tangu Lipumba na genge lake waendelee na shughuli za Chama? Zaidi ya hasara na kuturudisha nyuma mapambano yetu ambayo ndio msingi wa malengo ya Chama.

Kama vijana makini, hili pekee lilipaswa kuwa jawabu la kumkataa kivitendo, bwana yule...wakati ndio huu, vijana tunaweza kwa pamoja tuchukue hatua popote pale tulipo.

Anderson Ndambo
Mkuu, Idara ya Mipango na Uchaguzi,
JUVICUF-TAIFA

Hakuna maoni