NATO KUISHAMBULIA SYRIA
Shirika la kujihami la Magharibi la NATO lafahamisha kuunga mkono mashambulizi yanayoendeshwa na jeshi la anga la Marekani kwa ushirikiano na Ufaransa na Uingereza nchini Syria.
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema kuwa muungano wa NATO unaunga mashambulizi dhidi ya ghala ambazo zinaamika kuwa na silaha za kemikali nchini Syria.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa NATO, mashambulizi hayo yatapelekea kwa kiasi kikubwa kuathiri uwezo wa jeshi la Assad kuweza kushambulia raia kwa kutumia silaha zake za kemikali.
Katibu mkuu wa NATO ameendelea kusema kuwa washirika walikwisha kemea matumizi ya sialaha za kemikali hapo awali ni kufahamisha kuwa ni kinyume na makubaliano ya kimataifa.
Hakuna maoni