WATUHUMIWA 6 WA MAKOSA YA ULAWITI WASHIKILIWA NA POLISI
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu 6 kwa tuhuma za kuwakamata wanawake nyakati za usiku, kuwapora mali, kuwafanyia vitendo vya kikatili kuwalawiti na kuwapiga picha za utupu.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei na kusema kukamatwa kwa mtuhumiwa hao ni kufuatia matukio kadhaa ya aina hiyo yaliyo ripotiwa kutokea katika maeneo tofauti ya mji huo.
Amesema Watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia mbinu ya kudanganya kuwa ni askari kisha kuwapeleka sehemu wasizozijua na kuwatishia silaha na kuwapora mali zao na kisha kuwapiga picha za utupu.
”Akifika anatoa kisu, anatoa mapanga anaanza kumfanyia vitendo ambavyo ndivyo sivyo na kumpiga pichaza utupu” amesema Ulrich.
Hakuna maoni