Zitto Kabwe (Mb) awataka wazee wa ujiji kumaliza kazi huku akiaidi kumpeleka Nondo Uhamiaji
Mh. Kabwe amedai kwamba idara ya uhamiaji inatumika kisiasa, kutokana na mwenendo wao dhidi ya kijana na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam aliekumbwa na kadhia kadhaa mfululizo tangu apotee kimazingara na baadae kupatikana kimazingara pia.
amejikuta katika majaribu mapya chini ya mikono ya dola suala linalo tia wasiwasi kwamba, kuna mpango ovu unaopangwa dhidi yake.
Mh. kabwe ameguswa na jambo hilo kipekee sana na ameamua kulivalia njuga.
""Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji tarehe 20/4/2018 kwa mamlaka yangu kama Mbunge wa Kigoma Mjini ( Jimbo analotoka Abdul na wazazi wake na mababu zake ).
Wananchi wa Kigoma Mjini waliopo Dar watakaotaka kunisindikiza Mbunge wao kumpeleka Abdul huko sitawazuia. Anyways, Mwami lazima asindikizwe.
Siku hiyo Uhamiaji watatuambia kama Kigoma sio Tanzania ili tuwaombe wasio wa Kigoma warudi Tanzania maana haiwezekani waliowengi pasiwe kwao na wachache ndio iwe kwao.
Abdul Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana credentials ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Hii Serikali inatutafuta ubaya."Wazee wa Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo ya kipuuzi" amesema Zitto
"Idara ya Uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania. Sio kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma. Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana. Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa Uhamiaji na Serikali ya Awamu ya awamu ya Tano kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B." amesema Zitto
suala hili limeendelea kuchukua sura mpya baada ya kuibu tena bungeni, ambapo Mh. waziri wa mambo ya ndani alipoulizwa swali na kulikwepa na kushindwa kujibu swali hilo mahususi juu ya mwanafunzi huyu.
Hakuna maoni