UISHI KWA FURAHA PAMOJA NA MKE UMPENDAYE, SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO YA UBATILI, ULIZOPEWA CHINI YA JUA… Mhubiri. 9:9
Kumekuwepo na makosa mengi sana kwa Wakristo wengi na watu woote kwa ujumla, katika maisha ya ndoa ambayo yaliyo jengwa kwenye msingi mbovu wa ndoa yenyewe tangu mwanzo.
Kwamba, ndoa nyingi za watu, zimepatikana kutokana na sababu zisizo sahihi, na ambazo ndizo zimewapeleka wengi katika shimo kubwa na tanzi katika maisha yao ya ndoa na hata kuhatarisha uhai wa ndoa hizo mbali na kuangamia kabisa kwa ndoa hizo.
Moja ya sababu ambazo watu wamekuwa wakizitumia kama vigezo vya wao kuhalalisha maamuzi yao ya kuoa au kuolewa na fulani ni kama hizi..
1. Maono: kwamba, ni kawaida sana kuwasikia baadhi ya Watu wakisema kwamba "Bwana amenifunulia, Bwana amenipa maono" na hoja kama hizi ndio zinatumika kumhalalishia mtu kuamua kuoa au kuolewa na Fulani. Hii ni hoja potofu na inaweza kugharimu ndoa yako na maisha yako kwa ujumla.
2. Ushawishi wa ndugu na marafiki. Katika baadhi ya watu, kumekuwepo na mtego wa ushawishi wa ndugu na haswa wazazi na pia marafiki wa karibu katika kumfanya mtu aolewe au kuoa mtu fulani. Hoja hii ambayo msingi wake ni hulka za ndugu, jamaa kutoheshimu uhuru na utashi wa mtu binafsi ambao msingi wake ni Mungu mwenyewe ambae nae anaishia kutushauri tu na sio kulazimisha kuamua. {Zaburi 32:8; Yoshua 24:15}. Na imewagharimu wengi sana katika maisha yao.
3. Mtizamo wa jamii inayo kuzunguka. (Aibu). Wamekuwepo watu, ambao labda kutokana na hadhi za maisha yao kabla ya kuolewa au kuoa, wanajikuta katika aibu kubwa, kwamba mfano, akiolewa na fulani ambae ni masikini au kabila fulani, jamii au ndugu wanao mzunguka watamwonaje?? Hata kama huyo mtu ndie aliempenda. Na hoja hii imewaharibia wengi sana katika maisha yao, kwasababu hatuoi mtu ambae wengine wanamwonaje au watamwonaje, kwasababu huyo mtu tunakwenda kuishi nae sisi, sasa ukioa mtu ambae anawapendeza, mathalani wazazi wako, na wewe hujampenda, basi maisha yenu ya ndoa ni raisi sana kuwa mafupi.
4. Tamaa za mwili. Wapo watu ambao kutokana na tamaa zao za mwili, basi wanalazimika kuingia kwenye ndoa, ijapokuwa hili ni mojawapo ya sababu ya mtu kuoa au kuolewa, lakini halipaswi kuwa msingi wa maamuzi ya mtu kuingia kwenye ndoa. Kwasababu tamaa hukatika ndani ya dakika moja tu, baada ya tendo la kujaamiana, sasa kama msingi wako wa ndoa ulikuwa hapo, ukishafanya na tamaa ikakatika, basi utajikuta katika hali ya kumchukia huyo mwenza wako kuliko kitu chochote kile jambo ambalo linaweza kuigharimu ndoa yako. Kwahiyo hoja hii nayo ni dhaifu sana na haipaswi kuwa msingi wa maamuzi ya mtu kuingia kwenye ndoa.
5. Hali ya maisha. (Magumu au Mazuri). Wapo pia watu ambao wanataka kubadilisha maisha yao kwa kuoa au kuolewa na mtu mwenye uwezo wa kifedha au kimaisha. Aidha, wapo pia Wakristo ambao wanata kuolewa au kuoa mtu ambae anauwezo mkubwa sana katika mambo ya rohoni, kwamba yule fulani ni mwombaji, mhubiri, au mchungaji. Haya mambo mawili hayapaswi kutumika kama hoja ya msingi katika kukufanya uoe au uolewe na fulani japo si dhambi kama ukiolewa au kuoa mtu mwenye hali hizo nilizo zitaja. Na ni kwasababu hali hizi zote iwe ni za kimwili au kiroho, huweza kubadilika wakati wowote, na kama msingi wako lijengwa katika hayo, basi hali ikibadilika, inaweza kuvunja ndoa yako kabisa.
Sasa, baada ya hayo hapo juu, kwa kawaida unaweza kujikuta na maswali mengi sana kichwani, na pengine njia panda kwamba sasa kama hali ndio hiyo, sasa nifanyeje? Hiyo hoja ni ipi sasa ya kuzingatia?
UPENDO.
Maandiko yanatufundisha jinsi Mungu anavyojiusisha na maisha yetu, na namna tunavyopaswa kuenenda ili tusije tukaingia katika mateso makali na ambayo yanaweza kabisa kutuangamiza.
Hapo mwanzo Mungu alimuumba ADAM, na baada ya uumbaji huo, Mungu akaona kuna kitu kimepungua kwa ADAM, na ndipo akasema, "nitamfanyia msaidizi" { Mwanzo, 2:18} na ndipo Adam akalala usingizi na Mungu akamuumba EVA kutoka katika mwili wa Adam {Mwanzo, 2:21-22}..
Aidha baada ya Adam kufanya uasi kwa Mungu, kwa kula tunda ambalo Mungu alilikataza, Mungu akarejea kwa Adam na kumuuliza kwanini umekula lile tunda nililo kukataza? Adam akamjibu Mungu "Si huyu mwanamke ulie nipa" {Mwanzo, 3:12} Mungu aliheshimu kile alichokifanya, lakini pia alizingatia hoja ya Adam. Kwamba ni kweli mwanamke Eva hakuombwa na Adam bali yalikuwa ni matashi ya Mungu mwenyewe.
Ndipo Mungu akabdilisha sheria, na ndipo tunajifunza katika mandiko haya..Mhubiri. 9:9 ... UISHI NA FURAHA NA MKE UMPENDAE"" kwamba sio ukaishi na mtu nimpendae au Ampendae Mungu, No, mtu umpendae wewe, kwamba hata kama mimi simpendi, lakini kama wewe umempenda, basi ukaishi nae, na ndio maana hata kwa Samson, Mungu mwenyewe aliruhusu Samson amuoe Delila, mwanamke kahaba na msaliti. Ni kwasababu Delila lilikuwa chaguo la Samson na sio Mungu. Na Mungu akauheshimu uamuzi wa Samson lakini uamuzi huo mwishoni uligharimu maisha ya Samson.
Aidha, Mungu, katika Zaburi. 32:8, anasema atatushauri njia tunayopaswa kuiendea. Kwa kawaida ushauri ni hiari na huja pale ambapo anaetaka kushauriwa ameomba ushauri huo. Na huu ndio msingi wa kwanini tunamwomba Mungu, kwa habari ya mchumba na kwamba sisi kama wanadamu hatuna uwezo wa kumjua mwanadamu kiundani sana, kwasababu, mwanadamu anaweza akajifanya ni malaika wa nuru, {2wakorintho. 11:14} kumbe ni mbwa mwitu mtupu, sasa namna pekee ya kumjua huyu si kondoo bali ni mbwa mwitu, ni kwa Maombi, tunapo mwomba Mungu juu ya mke mwema au mumwe mwema, tunakuwa tunaomba ushauri na msaada kutoka kwa Mungu, na ndipo Mungu anatuonyesha ukweli wa mambo, kama tunaelekea kukosea au tumepatia. {Mithali, 31:10}
Yoote haya, Mungu ameyabadilisha kwasababu, ya namna Adamu alivyomjibu Mungu pale adeni, kwahiyo ukioa au kuolewa na mtu asiefaa, na ukajikuta umekuwa mzinzi, hakutakuwa na excuse mbele zake, na Mungu atakuhoji tu, na kama hutatubu basi adhabu yako iko palepale.
Mungu akasema, uishi na mtu umpendae...katika 2wakoritho. 13:1-5, tunajifunza maana ya upendo wa Kimungu, upendo wa Agape, kwamba upendo huvumilia yoote, hauesabu mabaya, hautakabari, hauoni uchungu, n.k. kimsingi upendo wa Mungu, ni upendo wa ajabu sana, ni upendo wa namna ya upofu. Mfano, katika Yohana. 3:16. Maandiko yanasema, kwa jinsi hii Mungu alivyoupenda ulimwengu, akamtoa mwanawe wa pekee. Lakini sehemu nyingine katika maandiko Mungu anasema "Macho yangu hayawezi kuangalia uovu" Mungu ni mtakatifu sana, kiasi kwamba ni najisi kwake kuutazama uchafu wa wanadamu, lakini kwa jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu, sio aliuangalia uchafu wa walimwengu, bali akauvua utukufu wake wa Mbinguni na kuuvaa mwili mchafu wa mwanadamu alieuumba yeye mwenyewe na akaja kuisha pamoja na sisi duniani, hakika upendo huu ni wa ajabu sana, ni kusema Mungu aliamua kuwa kipofu kwa Muda ili atusaidie sisi wanadamu waovu.
Aidha, katika {Wimbo Ulio Bora, 8:6}. tunajifunza kwamba, Upendo wa kweli una nguvu kuliko mauti, ni sawa na kusema Mungu alitupenda mpaka akamtoa mwanae wa pekee aje asulubiwe mpaka afe, akutwe na umauti kwa ajili ya wanadamu. Ndio maana si ajabu kusikia mtu amekufa kwasababu ya mapenzi, likiwa ni suala la Upendo wa kweli, kunaweza hata kugharimu maisha ya mtu.
Upendo, upendo wa Agape, ndio msingi wa ndoa. Lazima mtu unae taka kumuoa au kuolewa nae, lazima uwe umempenda kwa dhati na kwa pendo lisilo na unafki. {Warumi, 12:9}
Ni kweli kwamba, kwa watu tuliookoka, ni maagizo ya Mungu kwamba tuoe au kuolewa na mtu alie okoka. Lakini pamoja na kuzingatia hilo, ni lazima mtu huyo uwe umempenda kwanza, kinyume chake, achana nae, usije ukaingia mtegoni na shetani ataiharibu ndoa yako huko mbeleni. {2Wakorintho, 6:14}
Ikitokea umepata hayo yanayoitwa maono, ni lazima yapimwe na hoja hii kwanza, Je mtu huyo ameokoka kama wewe? pia je mtu huyo umempenda?? Upendo wa agape?? Kama umepata maono au ndoto juu ya kijana fulani lakini moyo wako haujampenda, tafadhali sana achana nae mapema, kabla hujaingia katika mateso makali sana.
Hivyo basi, ni heri kuoa au kuolewa na mtu ambae umempenda, na hujawai kumwona kwenye ndoto, maono, hujawai kushuriwa na ndugu na jamaa zako, sio kwasababu ya tamaa ya mwili, sio kwasababu ya mali, hakika utakuwa salama, lakini hata ukimwona live, lkn hujampenda achana nae kabisa.
Na katika mazingira haya, ndipo tunapolazimika kumwomba Mungu, kwasababu sisi kama wanadamu hatuwezi kumbaini mtu mwongo na aliye jificha kwenye pazia la kondoo kumbe ni mbwa mwitu.
Wakati mwingine tutajifunza namna ya kujua kwamba kama kweli hicho unacho kiita upendo ndicho upendo wa kweli? Je tofauti kati ta kumtamani na kupenda ni ipi? Utajuaje kwamba kweli umependa kwa dhati?
Hakuna maoni